AJALI; BASI LA TUMBUKIA BAHARINI.


TANGA.

Basi la Kampuni ya MOA linalofanya safari zake kutoka Tanga kupitia Pangani na kuvuka kwenye kivuko hadi Kipumbwi limezama wakati linatoka ndani ya kivuko cha MV Tanga ambacho kilikuwa kimefika mwisho wa safari eneo la feri ya Kipumbwi kikitokea Pangani.


Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah ambaye amefika eneo la tukio amesema hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha wala Majeruhi kwenye ajali hiyo kwakuwa Abiria walikuwa wameshuka na kukaa ndani ya kivuko kama ilivyo kanuni za siku zote za kivuko na kwenye Basi alibaki Dereva pekee yake ambaye pia aliwahi kuruka wakati Basi lilipofeli breki na kutumbukia majini.


Aidha kwa sasa juhudi za kulitoa Basi hilo ndani ya maji zinaendelea kufanyika.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.