Na Emmanuel Kawau.
Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu ambapo hatua hiyo inakuja kutokana na jitahada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akizumgumza na Waandishi wa Habari leo Julai 17, 2023 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax amesema Mkutano huo unalenga kujadili fursa za rasilimali watu pamoja na kubadilishana uzoefu baina ya mataifa ya Afrika katika Sekta ya Rasilimali watu.
"Tanzania imechaguliwa kuaandaa mkutano huu hivyo tunalinda sifa ya nchi yetu na sio kuchafua taswira ya nchi tunatambua umuhimu wa mkutano huu tutatangaza utalii, biashara, uwekezaji na vitu vingine."
"Mkutano huu utahudhuriwa na viongozi mbalimali, Wakuu na Taasisi za Kimataifa ambao utakuwa na washiriki 600 watakaoambatana na watu 1000 ambapo Julai 25 mwaka huu watakutana Mawaziri kujadili mambo mbalimbali pamoja na kutathimini na kuweka mikakati ya ushirikiano ambapo Julai 26 itakuwa ni kilele cha mkutano huo ambapo Wakuu wa Nchi za Afrika watakutana.” Amesema Stergomena.
Kwa upande wake Kamishina wa fedha kutoka wizara ya fedha Rashed Bade amesea Tanzania imewekeza zaidi katika elimu, afya na lishe ili kuzalisha rasilimali watu ambao ni mtaji mzuri kwa Taifa.
"Sisi, hii kwetu ni fursa kubwa kwani tutaweza kujifunza kutoka kwenye nchi mbalimbali mbinu wanazozitumia katika kukuza rasilimali watu," amesema Beda
Mkutano huo wa Rasilimali watu Afrika umeandaliwa na Bank ya Dunia (WB) na utafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam kwa siku mbili ambapo unatarajia kuanza July 25 na kukamilika July 26 .

Hakuna maoni: