Home
/
Unlabelled
/
MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI BARANI AFRIKA YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100%.
MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI BARANI AFRIKA YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100%.
Dar es salaam,
Na Emmanuel Kawau.
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika,kuhusu mtaji wa rasilimali watu ambapo maandalizi yake mpaka sasa yamekamilika kwa asimia 100%, utakaofanyika kuanzia Julai 25 -26, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Akizumgumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkutano huo ni muhimu mkutano huo ni sehemu ya utalii na itasaidia kuimarisha utalii wa Hotel,fukwe na vyakula vya kitanzania.
"Tutakuwa na wageni wasiopungua 1,200 ambao watakula,watalala na watatembelea maeneo mbalimbali,nipende kwa pamoja tuhakikishe maeneo yetu yanakuwa masafi na kusimamia usafi wa kaya hadi mitaa ma mji kwa ujumla ili wageni wanaoukuja Dar es salaam waondoke wakiwa na picha kubwa"
"Niseme kwamba ugeni huu ni wenu katika jiji hili la maraha la Dar es salaam ambalo Afrika inalitumia katika kuhakikisha Azimio juu ya hali ya ufanyajikazi wa kizazi cha kiafrika unaimarika kwa manufaa ya Bara letu la Afrika.Tanzania ni nchi ya mfano kwenye mambo mengi,na inatumika tena kwa mara nyingine kuandaa Azimio la Dar es salaam juu ya rasilimali watu".Amesema RC Chalamila.
Ameongeza kuwa wageni kutoka Mataifa zaidi ya 30 Barani Afrika watawasili Jijini Dar es salaam na kuhudumiwa na zaidi ya hotel 40 huku wajasiriamali zaidi ya 100 kushiriki kwenye mkutano huo kwa kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa hususani za utamaduni wa kitanzania.
RC Chalamila pia amewataka wakazi wa Jiji la Dar es salaam na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa ya kibiashara zilizopo kupitia mkutano huo na kuhakikisha "Lengo la Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam ni kuhakikisha kila mgeni aliyekuja Dar es salaam anaacha Dola zake hapa".
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JNICC Ephraim Mafulu amesema maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika ikiwemo kumbi zote zitakazotumika,vifaa vya maswaliano,vyumba vya kutafsri lugha mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.
Aidha amesema kuwa Tanzania inashika nafasi ya Tano Afrika kuwa muandaaji wa mikutano yote inayofanyika katika Bara la Afrika sawa na Asilimia 13% ya mikutano yote.
Baadhi ya picha zikionesha maeneo mbalimbali ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) uliondaliwa tayari kwa mkutano huo.







Hakuna maoni: