Dar es salaam.
Wadau na wanamuziki zaidi ya 1000 kutoka zaidi ya mataifa 50 Duniani wanatarajia kukutanishwa katika Tamasha la Muziki la ACCES linalotarajiwa kufinyika Novemba 9-11, 2023 Jijini Dar es salaam.
Kutokana na ujio wa Tamasha hilo
Wasanii nchini wametakiwa kutumia fursa za tamasha hilo na majukwaa mengine kupata fusra ya masoko ya kazi zao wanazozifanya pia kukutana na wadau muhimu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa hiyo Jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa BASATA Kedmon Mapana Amesema Tanzania imebahatika kuwa mwenyeji tena wa mkutano na Tamasha la music la ACCES na kutoa fursa nzuri kwa wasanii wa ndani kupata uzoefu mpya na kuweza kupata nafasi ya kukutana na kishirikiana na wasanii wa nje kwa urahisi.
"Mkutano huu utahudhuriwa na mataifa mengi na wameona Tanzania ni mahali sahihi na waliangalia kuwa Watanzani ni wakarimu wanapenda mziki ni nchi yenye amani na usalama huduma. zao ni nzuri " Dkt Mapana
Kwa upande Mkurugenzi wa Taasisi ya “Music in Africa Foundation na ACCES Eddie Hatitye ambaye ni muandaaji wa mkutano huo amesema fursa pekee ya muhimu kupatikana pamoja na masoko ya muziki pia kupitia fursa hiyo wasanii wote Tanzania wakiwemo chipukizi na watafanikiwa kuonyesha vipaji vyao.
" Lengo la tamasha hilo ambalo linandaliwa na Taasisi ya Music in Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania ni kuwasaidia wanamuziki kutambuana na kuonyesha uwezo wao wa kuimba pamoja nakufundishwa namna ya kuchangamkia fursa za masoko"amesema Eddie
Tamasha hilo la ACCES linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wa muziki zaidi ya 1000 kutoka zaidi ya mataifa 50 duniani ambapo kwa Tanzania linafanyika kwa mara ya pili pia mwaka jana lilifanyika Novemba 24-26, 2022 jijini Dar es Salaam
Naye Mratibu wa Mkutano huo upande wa Tanzania Mandolin Kahindi amesema kwa mwaka jana walifanikiwa kwa aslimia kubwa hivyo mkutano huo unakuwa wa tofauti unakuwa na wadau muhimu ukiwemo wanaonunua mziki kwa njia ya mitandao wanakuwepo ambapo hao wadau kama hao huwezi kukutana nao peke yao hivyo uhudhirie na
Aidha ametumia wasaa huo kuwakaribisha watu wote hususani wadau wa muziki nchini kuhudhulia Tamasha hilo kwani ni bure na litafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam.


Hakuna maoni: