Dar es salaam,
Na Emmanuel Kawau.
Mabinti na warembo Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18-35 wametakiwa kuchangamkia fursa na kushiriki shindano la Instaqueen Tanzania ambalo linafanyika kidigital.
Akizungumza na waandishi wa habari leo September 20/2023 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Insta Queen Tanzania Maximilian Donald amesema shindano hilo la urembo ni la kidigital ambalo linasherehekea uzuri,vipaji na weredi binafsi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii hususani Instagram.
"Instaqueen inalengo la kubadilisha mawazo ya vijana katika kutumia mitandao ya kijamii kwa maendeleo chanya kwao na kwa jamii inayowazunguka,pia Instaqueen inashiriki katika kusherehekea uzuri wa asili,vipaji na ubunifu" Amesema Maximilian.
Maximilian ameongeza kuwa Instaqueen inatumia nguvu ya mitandao ya kijamii, ikifanya iweze kupatikana kwa hadhara ya ulimwengu na kuwawezesha watu mbalimbali kushiriki shindano popote pale walipo.
Kwa Balozi wa Instaqueen, Meena Ally amesema kuwa shindano hilo litakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza atapewa Zawadi ya shilingi milioni 3, wapili shilingi milioni 2, watatu shilingi milioni 1 na wote watapatiwa msaada wa masomo na kazi za kudumu.“Mtu yeyote anayekidhi vigezo na masharti ya Instaqueen anaruhusiwa kushiriki mashindano ya Instaqueen, ikiwemo kigezo cha umri wa miaka 18-35, uraia wake awe Mtanzania, awe Mwenye maadili na picha zake ziwe za kimaadili,”.
Pia amesema washiriki wanaweza kuanza kutuma picha zao Tatu "full short,medium short & half short kwenye Whatsapp namba +258842555649 pia wanatakiwa kutembelea kurasa ya Instagram ya @instaqueentanzania.
Kwa upande wake Dkt. Kumbuka ambaye ni Balozi mwingine wa shindano hil amesema Instaqueen inawasaidia washindani kujiamini, kuendeleza vipaji vyao katika tasnia ya urembo, kujifunza mengi kuhusiana na masuala ya urembo, na kupata kutambuliwa katika tasnia ya urembo na mitindo na cha pili Instaqueen inatoa fursa za Kazi na kuongeza ujuzi.Ameongeza kuwa shindano hilo litafanyika kwa uwazi na Watanzania wenyewe ndio watakaoamua nani apite katika washiriki watakaojitokeza kwa kupiga kura kupitia kurasa ya @instaqueentanzania.
"Warembo wote Tanzania nzima ajalishi upo wapi,uwe Manyara,Mbulu,Mara,Arusha,Mwanza,Kigoma wewe jitokeze tumia fursa hii ya kidigital kama hauna simu janja azima kwa ndugu /jamaa au rafiki na uweze kushiriki kwa kutuma picha zako na kifwatilia kila linalojiri kwenye kurasa zetu kwenye Instagram".
Shindano hilo la Instaqueen fainali yake inatarajiwa kufanyika Desember 5 mwaka huu,baada ya washiriki kupita kwenye mchujo na kubaki na top10.



Hakuna maoni: