CHALAMILA AWATAKA WAMILI WA BAA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA KUFICHA WAHARIFU.



DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Wamiliki wa Bar, Night Club na Grosari, kuwa Mabalozi wazuri wa amani katika maeneo hayo ya starehe ili zisiwe Ofisi za kuwalinda Vibaka na Majambazi wanayoiharibu Jamii.

Ameyasema hayo Katika Mkutano wake na Wamiliki wa Baa Kwa lengo la Kujadili na kuepena maelekezo ya utendaji kazi wao Katika kuelekea kipindi Cha Sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya 2024.

Chalamila amesema kumekuwa na Mamalamiko mengi yanayowakilishwa na Baadhi ya Wakazi wanaoishi karibu na maeneo wanayofanyia biashara Wamiliki hao ambapo kero kubwa ni kelele zilizopitiliza ambazo zinawasababishia matatizo ya Afya.

Wakati huo huo amewataka Askari WA Jeshi la Polisi Kufuata kanuni na Sheria zilizoainishwa na Jeshi Hilo bila kukiuka Sheria hizo.

Nae Mwenyekiti WA Chama Cha Wamiliki wa baa na kumbi za Starehe Nchini Mponjoli Mwakabana amemuomba Mkuu WA Mkoa huo waiangalie vizuri Sheria ya 1968 inayowataka wafungue biashara Zao sa kumi jioni na kufunga saa Tano usiku ambapo Sheria hiyo inawasababishie kushuka Kwa Uchumi wao na kuisababishia Serikali kutokusanya Kodi.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.