Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amesema Uwepo wa Kampuni changa nchini unachagiza kasi katika mapinduzi ya nne viwanda Dunia ambayo yanategemea zaidi teknolojia.
Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa pili Tanzania Startup Association (TSA) uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema kampuni changa zinamchango mkubwa katika kutoa bunifu mpya kwenye sekta mbalimbali ambazo zinahitajika katika Dunia ya sasa.
Ameongeza kuwa hivi sasa kuna sera mpya ya kampuni changa inayotarajiwa kutolewa kwa umma na kutoa maoni yao na baadae kufikishwa bunge ili iweze kuwa sheria na kuweza kuzisaidia kampuni changa nchini.
"Hatutaki kwenda kudhibiti tunataka kuwe na teknolojia inayoenda na maadili yetu, kusema unadhibiti huwezi kwamaana teknolojia kila siku inazidi kukua na kuzaliwa mpya".
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Startup Association amesema sera ya Startup inalenga kuweka mazingira bora kwa kampuni changa, wajasiliamali, wafanyabiashara na wabunifu nchini.
Tanzania Startup Association hii leo katika mkutano huo imetoa Tuzo ya heshima kwa watu waliotoa mchango mkubwa katika sekta ya maendeleo ya teknolojia nchini hususani sekta ya fedha, uwekezaji na biashara akiwemo Balozi Ami Mpongwe na Aliyewahi kuwa Gavana wa Bank Kuu Tanzania Prof Beno Nduru




Hakuna maoni: