DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan mapema hii leo December 20/2023 amefanya mazungumzo na Bodi na menejimenti ya Tanzania Startup Association (TSA) iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na Wajumbe aliofuatana nao Ikulu Jijini Dar es salaam.
Ambapo wamepata wasaa wa kuzungumza kwa kina kuhusiana na masuala ya Sekta ya Startup na kwa namna gani yana mchango katika ajira, kazi, uwekezaji na uchumi nchini.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kutatua changamoto za Startups ambazo TSA wameziwasilisha kwake.
Aidha TSA, inapongeza jitihada na utayari wa serikali kuboresha mazingira wezeshi ya kibiashara kwa startups.



Hakuna maoni: