Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori( TAWA ) wametoa mafunzo kwa sekta ya Benki na Mawasiliano kwa lengo la kudhibiti vitendo vya ujangili Nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Semina hiyo iliyofanyika leo December 7/2023 jijini Dar es salaam Meneja Miradi ya Kuhifadhi Maliasili kutoka TPSF Bw.Godfrey Mondi Amesema kumekuwepo na biashara haramu ya Wanyamapori,hivyo sasa ni wakati wa taasisi za serikali na sekta binafsi kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutokomeza ujangili na biashara haramu ya Wanyamapori nchini.
" Leo TPSF tumeshirikiana na TAWA kufanya semina hii kwa washiriki wa sekta ya benki na taasisi za Mawasiliano kwani hawa ni wadau muhimu ambao tunashirikiana nao katika kupambana na hali ya ujangili,mradi huu wa kuhifadhi Maliasili unafanyika kwa muda wa miaka mitano na umefadhiliwa na wenzetu wa USAID". Amesema Mondi.
Kwa upande wake afisa Wanyamapori kutoka TAWA ,Dolorosa Maricky amesema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa sekta ya Bank kwani majangili na wafanyabiashara haramu hutumia Benki kufanya miamala mbalimbali kwaajili ya kuwezesha shughuli zao." Lazima kuwepo na ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ,hivyo warsha kama hizi zinasaidia kuleta umoja kati ya serikali na Sekta binafsi katika kuhakikisha tunapambana na ujangili" Amesema Dolorosa.


Hakuna maoni: