DAR ES SALAAM.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni iliopo Jijini Dar es salaam imeanza kutekeleza agizo lililotolewa mwaka 2021 na Rais Dr Samia Suluhu Hassan linalozitaka Shule za Msingi kuanza kutoa Mafunzo ya Mtalaa Mpya ulioboreshwa ili kuwawezesha Wanafunzi kuibua vipaji vyao vitavyowawezesha kuwa mahiri Katika Jamii.
Ameyasema hayo Afisa Elimu Msingi wa Kinondoni Theresia Kyara January 9/2024 Katika Semina iliowakutanisha Walimu wa Shule hizo kwenye Halmashauri hiyo ili kupewa Mafunzo ya namna ya utekelezaji Mtalaa huo.
''Waalimu watajikita kuwa kiini na Uhai Nchini na Leo tumeanza zoezi hili linalohusisha namna ya kutekeleza Mtalaa hasa Katika masomo ya vitendo".
.
Afisa huyo amesema mafunzo hayo yanaendelea Kwa Walimu wa darasa la awali, la Kwanza na la tatu ambapo Wanafunzi wanajengewa umahiri ulioboreshwa na kuacha masomo yasiokuwa na tija hivyo Kinondoni nzima imeshaanza utekelezaji huo.
Kyara amesema Wanafunzi wataanza darasa la awali akiwa na umri wa miaka mitano na la Kwanza akiwa na umri wa miaka 6 kwani Serikali imejipanga kutekeleza Mtaala huo
"Tutakuwa na Walimu zaidi ya 600 watakaofundisha Mtaala huo Katika madarada hayo ambapo Mtalaa umejikita kwenye ujuzi mbalimbali wa kujitegemea ikiwemo ufundi uchoraji na upambambaji na uyatusaidia umahiri WA utendaji kazi wetu.
Amesema Serikali imejipanga Katika kuhakikisha Mtalaa huo unatekelezwa Kwa haraka zaidi na kuongeza kuwa tayari vifaa vimeshaandaliwa ili kuanza utekelezaji wake na Kinondoni imeshakuwa tayari kutekeleza agizo hilo Kwa asilimia 100 hadi ifikapo 2027.


Hakuna maoni: