Na Mariam Muhando
Dar es salaam,
MJUMBE wa Kamati Kuu Taifa ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam Sudi Kassim Sudi amewataka Madiwani wa Chama hicho kuhakikisha Wanawapa Semina Wajumbe ili CCM ishinde Kwa Kishindo Katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Mwaka huu na Mkuu 2025.
Mjumbe huyo ametoa agizo hilo January 11-2024 Katika Mkutano uliowakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya wazazi CCM Kata ya Charambe iliopo Temeke Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kuangalia uhai wa Jumuiya na kuona namna ya kuwaingiza na kuwasajili Wanachama Wapya wa Chama hicho.
Sudi amesema ipo haja ya Madiwani kuwapa Semina Wajumbe hao ili Waweze kuwa na uelewa wa kuhakikisha Chama Kinashika Dola ifikapo 2025.
""Lazima Jumuiya ijipange ili Chama kipate ushindi na tumegundua Kuna changamoto mbalimbali Katika jumuiya ikiwemo Wajumbe kutopewa Semina hivyo changamoto hiyo tunakwenda kuitatua kwani Viongozi Wengi hawakupatiwa semina inayowaelekeza majukumu yako ".
Wakati huo huo amemtaka Katibu Kata wa Jumuiya hiyo Jumanne Madebwe kuhakikisha kadi za CCM Zaidi ya 1300 zinapatikana ili zikatumike kuwasajili Wanachama Wapya wanaotokana na Jumuiya hiyo ambapo watasajiliwa siku ya Semina hiyo inayotarajiwa kufanyika kabla ya February mwaka huu.
Kwa upande wake Katibu huyo Jumanne Madebwe amesema kuna Viongozi mbalimbali wameahidi kuwapa kadi elfu1300 akiwepo Diwani waViti maalum Chikole Abdallah Diwani Kata ya Charambe Twahil Kamona na Viongozi wa Serikali za Mtaa ambapo atakapo zipata atazigawa kadi mia 325 Kila tawi na kuwasajili Wanachama Wapya ili kuongeza idadi ya Jumuiya hiyo kwani ndio mtaji wa CCM.
Madebwe amesema wanategemea hadi wiki ijayo atatoa maekekekezo Kwa Viongozi mbalimbali ili kuhakikisha nafasi ambazo ziko wazi zinakuwa na Wanachama hai ili Jumuiya hiyo iweze kupiga hatua ya kuhakikisha Chama Kinashika hatamu.
Nao Madiwani hao wamesema ni maelekezo ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan ya kuwapa Semina Wajumbe wa ngazi zote kwenye Kata ya Charambe Kwa Kushirikiana ambapo Moja ya jukumu la Jumuiya hiyo ni kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwemo kuboresha Sekta mbalimbali.
Diwani Kamona amesema hadi Sasa wanaendelea na zoezi la harambee Kwa ajili ya kuchangia madawati Katika Shule ya Msingi ambayo ukomo wake ni January 31 sambamba kuboresha miundombinu ya barabara zenye kiwango Cha zege hususani barabara ya pazi na kilamba.



Hakuna maoni: