Dar es salaam,
Na Emmanuel Kawau.
Bodi ya Sukari Nchini (SBT) imesema Serikali imeshachukua hatua za kukabiliana na uhaba wa Sukari Tanzania ikiwa ni pamoja na kuagiza Tani 50,000 za dharula kutoka nje ya nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Prof Kenneth Bengesi amesema pamoja na hatua hiyo pia Serikali imeagiza kuanza kwa uzalisha wa sukari katika viwanda ambapo awali viliacha kutokana na changamoto ya mvua kuzidi hivyo kuharibu Miundombinu ikiwa ni pamoja na miwa kupungua kiwango cha sukari kutokana na maji mengi yaliyopo.
"Kwanza tumerejesha viwanda kuzalisha hata kama ni kidogo lakini viendelee kufanyakazi na sukari nyingine Tani Elfu Hamsini imeagizwa na itaingia kuanzia kwenye Tarehe 22 January hii" amesema Prof Bengesi.
Ameongeza kuwa Kuanzia November 2023 uzalisha wa sukari ulishuka na kufikia tani 345,000 pekee ambazo hazitoshelezi mahitaji ya kawaida ya nchi ambayo ni tani Laki Tano na Ishirini (520,000).
"Malengo yetu ni kuzalisha tani 555,000 ili tuwe na akiba ya sukari ya kutosha lakini kutokana Msimu huu wa mvua za El nino tumeshindwa kufikia lengo ndiyo maaana tuna uhaba wa sukari lakini Serikali yenu sikivu ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imechukua hatua stahiki za kukabiliana na changamoto hiyo".
Aidha katika hatua nyingine Pro Kenneth Bengesi amesema wamebaini uwepo wa wafanyabiashara waotumia vibaya changamoto hiyo na kuanza kupandisha bei kiholela wakati wafanyabiashara hao wakiipata sukari kwa bei chini.
"Bodi inatambua kuwa kila mkoa unatofautiana bei ya sukari hivyo wafanyabiashara wanaopandisha bei kwa maslahi yao binafsi tofafauti na bei halali ya mkoa huo, tunategemea kuoana sukari ikiuzwa kwa bei za kawaida za tokea awali kuanzia 2500-3200 kwa Kilo moja kulingana na mkoa"
Aidha amesema hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa Wafanyabiashara watakaobainika kwenda kinyume na taratibu zilizopo za kuuza na kununua Sukari nchini.

Hakuna maoni: