WAZIRI MASAUNI AWAHAKIKISHIA WATANZANIA POLISI KUIMARISHA ULINZI NA USALA NCHINI .


Na Marim Muhando,

Dar es salaam.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni amewahakikishia Watanzania kuwa Hali ya Usalama Nchini imeimarika ambapo Jeshi la Polisi limefanya tathmini Kwa yale yote Wizara ilioyaagiza Katika kuhakikisha wanamaliza mwaka 2023 salama Kwa kutokuwepo matukio ya kiuhalifu.

Waziri Masauni ameyasema hayo Leo Januari 4, 2024 mara Baada ya kukutana na Wandishi wa Habari Kwa lengo Kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu Usalama na Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya Wizara hiyo.

"Nalipongeza Jeshi la Polisi kwani Nchi haiwezi kuwa salama bure bure, watu wako kazini. Jeshi linahakimisha Raia na Mali zao wanakuwa salama" Amesema Masauni

Masauni ameongeza kuwa kufuatia agizo la Amiri Jeshi Mkuu Nchini Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Jeshi la Polisi lijiimarishe Katika utendaji kazi wake, Amesema Rais aliamua kuunda Taasisi ya haki jina, matumizi ya tehama ambapo lengo ni Watanzania wapate huduma Bora ili kuepusha malalamiko.

 "Hatudharau mtu Serikali ya Watu na maslahi ya Watu nimeshuhudia malalamiko mengi yaliowagusa Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la Polisi tumeyafanyia tasmini yote hayo" Amesema Mhandisi Masauni.

Wakati huo huo amewahakikishia Watanzania kuwa Hali ya Usalama inazidi kuimarika na Jeshi Hilo linatekeleza majukumu ya Msingi Katika kumlinda Raia na mali zake ambapo Matukio yote ya kihalifu yanayojitokeza hatuna mbalimbali za kisheria zinazidi kuchukuliwa Kwa yeyote atakae kiuka.

"Mwenye nafasi yeyote Serikalini ama Kampuni, Nyazfa au Kiongozi na anaefanya kazi kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amezungumzia Uhalifu unaofanywa na Kikundi cha Vijana Panyarodi wanaotumia silaha mbalimbali za Jadi Kwa kuwajeruhi Wananchi ili Waweze kuwapora Mali Zao ambapo Kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria Hivyo Jeshi litazidi kuwashughulikia. 

 " Nguvubwa wanayoitumia Panyarodi inapekekea Askari wa Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya ziada ili kuwadhibiti wasiweze kuendeleza na uhalifu" Amesema IGP Wambura

Kwa mwaka huu 2024 wamepeana maelekezo ya kuhakikisha wanaliimamarisha Jeshi la Polis Nchini Kwa kufanya kazi Kwa weledi.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.