DAR ES SALAAM.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Januari Makamba amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utoajia wa maoni kuhusu masualua mbalimbali yanayohusu maswala ya kitaifa na kimataifa.
Makamba ameyasema hayo leo Januari 9,2023 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kukusanya maoni ya wadau mbalimbali kuhusu mapendekezo na Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya nje ya mwaka 2001 ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wadau mbalimbali ikiwemo wanasiasa Asasi za kiraia viongozi wa dini kushirikishwa wa kutoa maoni yao mahsusi katika mchakato wa marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.
" Nchi ya Tanzania kama yalivyo Mataifa mengine,ambayo nchi zao zinavyokabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki wake kwenye jukwaa la kimataifa,hivyo ni vema kuwa na sera madhubuti ambayo ni muhimu katika kutumia ipasavyo fursa hizo na kukabiliana na changamoto ambazo zitajitokeza,”amesema Waziri Makamba
Pia amesema ni muhumi kupata maoni ya sera hiyo ili kuwezesha taifa kunufaika ipasavyo na fursa zitokanazo na ushirikiano wa kikanda na kimataifa hasa utekelezaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi kwa maendeleo endelevu na Mustakabali wa Taifa pasipo kuathiri wananchi wake.
Aidha amesema ndani ya kongamano hilo wadau hao watapata fursa ya kuelewa kwa kina masuala muhimu yaliyomo katika sera ya mambo ya nje ikiwemo misingi ya Sera zao na malengo yake.
”Pia wataweza kupata uelewa wa historia ya sera ya mambo ya nje tangu kupatikana kwa uhuru hadi ilipofika mwaka 2001 ambapo utekelezaji wa sera ulianza mwaka 2001 hadi sasa yanafanyika mapitio ya sera hiyo,”amesema.
Waziri Makamba ameongeza kuwa katika kongamano hilo,wizara yake inapenda kusikia kutoka kwa wadau jinsi wanavyoona marekebisho yaliyofanyika katika sera na ni maoni gani waliokuwa nayo kuhusu njia zitakazochukuliwa kufikia malengo wanayotamani kufikia.
Kwa upande wake mmoja wa Viongozi wa Kisiasa waliohudhuria Kongamano hilo Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Nchin(TCD) Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwa sikivu kutokana na kuwashirikisha Wananchi wake katika utoaji wa maoni katika baadhi ya mambo muhimu ikiwemo masuala ya urekebishaji wa sheria.


Hakuna maoni: