DAR ES SALAAM.
Shirika la kazi Dunia (ILO) Limeihakikishia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuwaongezea uwezo wafanyakazi wake kwa kuwapa elimu mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano kati ya ILO NA TUCTA Mkurugenzi Mkuu ukanda wa Afrika Fanfan Rwanyindo Kayirangwa Amesema wanaipongeza TUCTA kuona haja ya kuongeza ulewa katika maswala ya jinsia, wanawake na makundi maalumu eneo ambalo ILO Linasimamia kikamilifu kuhakikisha kunakuwa na haki sawa kwa wote kwenye maswala ya kazi na ajira.
Ameongeza kuwa kwa pamoja wadau wote wa Maendeleo wanapaswa kupigia kelele swala la kushimu matakwa ya jamii (social justice) pia kazini kunapaswa kuwepo na majadiliano na makubaliano kati ya mwajili na mwajiliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika la kazi Dunia ILO ukanda wa Afrika Mashariki Bi Caroline Mogall amesema kutokana na mwangaza unaooneshwa na Tanzania kutokana na kauli mbalimbali za kiongozi Mkuu wa Nchi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ILO inatoa kipaumbele kikubwa kwa Tanzania kwani imeonyesha kuheshimu matakwa ya jamii(social justice).
Nae katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Hery Mkunda amesema wamewaomba ILO kuwaongezea uwezo Vyama vya Wafanyakazi Tanzania katika eneo la maswala ya wanawake kwani kumekuwa na uachishwaji wa kazi kwa wanawake wanaokaribia kujifungua au baada, hivyo kuwakosesha haki zao,
Ameongeza kuwa ajira za watoto ni moja wapo ya changamoto iliyopo nchini hususani katika Maeneo ya viwandani na vijijinia hivyo TUCTA kwa kushirikiana na wadau wengine wanajipanga kuandaa mpango maalumu kuondoa changamoto hiyo.

Hakuna maoni: