MSTAHIKI MEYA OMARI KUMBILAMOTO KUFUNGUA DUKA LA VIATU L.A. KAMPUNI YA BEST BRAND DISTRIBUTOR




Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Ziara Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutembelea nchi mbalimbali na kueleza fursa zilizopo Tanzania matunda yake yameonekana kutokana na Wafanyabiashara kutoka India kuonesha nia ya kuwekeza kibiashara na kujenga Viwanda vya kuzalisha bidhaa zao nchini .

Ameyasema hayo leo Mstahiki Meya wa Jijini Dar es salaam Omar Kumbilamoto wakati wa Ufunguzi wa tawi mpya la duka la viatu la.Kampuni Best Brand Disribitor ya linalojihusisha na Uuzaji wa viatu Relaxo Posta Mtaa wa Mororogoro / Samora ambapo amebainisha kupitia wawekezaji hao itasaidia kuzalisha ajira kwa vijana kwani lazima watahitajika wasambazaji hivyo na wale watakaonunua kwa jumla.kuuza rejaraja.

"Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa kuiweka.mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje hivyo kuwepo kwa wawekezaji hao nchini ni ishara tosha kuwa usalama upo wa kutosha na Kesho la polisi kumekuwa likifanya kazi usiku na mchana bila kuchoka " amesema Meya

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Best brands kupitia Khalid Mohammed Salim amesema Kampuni imejipanga kuhakikisha kufungua katika 20 na kujenga Kiwanda kitakachozalisha bidhaa zake nchini Tanzania ili kusaidia kuwafikia wateja wake nchi mzima na kuanza kugawa ajira kwa vijana zaidi ya 50 .


Hata hivyo amesema wanaishukuru Mungu ambapo mpaka sasa wamedukua 3 katika maeneo ikiwemo Mlimani city Clock tower na Mtaa Samora hivyo tutahakikisha tunavika mpaka Tanzania hata na Zanzibar Wateja wote wanakaribishwa kwani Maduka hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1 asubuhi hadi usiku.


"Kipekee tumepata maombi mengi ukizingatia viatu vyetu tumelenga zaidi upande wa kimichezo hivyo wanamichezo wengi wanapenda kupata viatu vyenye ubora zaidi ndio maana tukawiwa kuendelea kufungua matawi katikati ya mji hili la leo tumezindua ni la tatu na tuna mpango wa kufungua maduka 20 sanjari na ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa viatu hivyo ili kuwafikia wateja wao kwa haraka kutokana na ubora wa viatu hivyo."

Pia Salim ameongeza kuwa viatu vyao vinayozalishwa vimesheheni viatu kwa rika zote na sehemu mbalimbali eza mahususi ikiwemo kwa matumizi ya mashuleni,hospitalini na sehemu zingine zenye matumizi ya viatu.

Aidha amesema Kampuni hiyo imetoa ofa ya kwa wale wenye nia ya dhati kuuza bidhaa za kampuni hiyo watagharamiwa fremu za biashara ili kuendelea kuzitangaza bidhaa hizo.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.