Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutaarifu umma kuhusu maboresho ya Kitita cha Mafao kwa wanachama wake ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi tarehe 1 Machi, 2024.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu Berna H. Konga Kitita cha mafao ni orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu. Maboresho ya mwisho ya kitita cha mafao cha NHIF kinachotumika sasa yalifanyika Juni, 2016 takriban miaka nane iliyopita na hivyo kuwepo kwa umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali kama zinavyoanishwa kwenye taarifa hii.
"Maboresho ya kitita cha mafao yanalenga Kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuwepo awali; ii. Kufanya maboresho ya huduma na gharama zake kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko; iii. Kuwianisha Kitita cha Mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wanufaika wa Mfuko".
Ameongeza kuwa NHIF iliyoanzishwa kwa Sheria Sura 395 kwa lengo la kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa makundi yanayosajiliwa na moja ya jukumu lake ni kufanya mapitio ya Kitita cha Mafao kwa lengo la kuhakikisha kinaendana na mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika sekta ya Afya nchini na kwa mujibu wa tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko kama inavyoainishwa kwenye kifungu cha 39A cha Sheria hiyo.
Mfuko umejuisha maoni na mapendekezo mbalimbali ya Wadau
Kutekeleza ushauri wa Taarifa ya Mapendekezo ya Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2021 na vi. Kuimarisha udhibiti katika mianya ya udanganyifu
Konga amebainisha kuwa mfuko ulianza zoezi la kufanya marejeo ya kitita kuanzia mwaka 2010 Hata hivyo utekelezaji wa kitita kipya haukufanyika kutokana na uhitaji wa kuhusisha wadau zaidi ili kuwa na uelewa na maoni zaidi kuboresha kitita hicho.
Aidha Maboresho ya Kitita cha Mafao Kufanyika kwa Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko na kutekeleza mapendekezo yake ambapo tathmini ya mwisho ilifanyika Juni, 2021;
Jumla ya dawa 736 zimefanyiwa mapitio kwa kuzingatia bei za soko na gharama za uendeshaji na wastani wa faida. "Hii itandoa changamoto ya wanachama kukosa baadhi ya huduma za dawa kutokana na changamoto ya bei.Kuongeza dawa mpya 247 ambazo zinatokana na dawa mpya zilizoko katika Mwongozo wa Orodha ya Dawa Muhimu za Taifa (NEMLIT)".
Hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama.Kuzingatia mabadiliko katika ngazi za matumizi ya dawa kama zilivyoainishwa katika NEMLIT. Maboresho haya yataongeza upatikanaji wa huduma za dawa katika vituo vya ngazi ya msingi mfano dawa za matibabu ya shinikizo la damu na kisukari, Huduma za Upasuaji na Vipimo
Pia Gharama za vipimo 311 na huduma za upasuaji zimefanyiwa mapitio kwa kuzingatia bei za soko katika ununuzi wa vifaa na vitendanishi, gharama za uendeshaji na wastani wa faida.
Hii itaondoa changamoto ya Kukosekana kwa huduma za vipimo na upasuaji kutokana na changamoto ya bei.
Pamoja na hayo maboresho hayo Kuongeza wigo wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za upasuaji na vipimo katika hospitaji za Rufaa ngazi ya Kanda na Taifa.pia itarahisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya saratani, upasuaji wa mifupa, upasuaji wa moyo katika hospitali si za Taifa tu bali hata hospitali za Kanda hivyo kusogeza huduma karibu zaidi na maeneo ya wananchi.
Mfuko unaendelea kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa wadau wake hasa wanachama na watoa huduma katika kufanikisha utekelezaji wake.

Hakuna maoni: