Na Emmanuel Kawau.
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) hii leo,limezindua rasmi Treni ya umeme ya Abiria kutoka Stesheni Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.
Safari hiyo ilianza mnamo mida ya saa nne na Nusu na kuwasili Mkoani Morogoro mida ya saa sita na nusu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja kadogosa amesema Usafiri huo wa Treni utatumia umeme wa kawaida kutoka TANESCO na wanatarajia kuanza safari za abiria hivi karibuni.
Aidha amewatoa wasiwasi Watanzania wanaodhania kuwa umeme ukikatika utaweza kuleta athari kwa Treni hizo kuwa sio kweli umeme wake umeunganishwa kutoka grid ya taifa hivyo si rahisi umeme kukatika kwenye njia ya Treni.
Ameongeza kuwa katika majaribio hayo walimeambatana pamoja na Msemaji wa Serikali,wasanii, waandishi wa habari,wahariri na baadhi ya wafanyakazi wa TRC.
Treni hiyo inauwezo wa kutembea Km/h100-160.





Hakuna maoni: