DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wa UWT – Taifa Jokate Mwegelo amewataka wanawake kujitokeza kugombea katika uchaguzi mwaka 2024 wa serikali za Mitaa na Vijiji, na uchaguzi mkuu 2025 ili kuhakikisha idadi ya wanawake viongozi inaongezeka.
"UWT itahakikisha inahamasisha Wanawake wanajitokeza kwa wingi kugombea na kushika nafasi za Uongozi kuanzia Vitongoji, Vijiji na Mitaa.”
Ameongeza kuwa chini ya Mwenyekiti Mama Mary Chatanda (MCC) watahakikisha mwanamke akigombea atapitishwa na Chama na watampambania ashinde kwani UWT inasema “mwanamke usijione mnyonge na usijione upo peke yako, Jeshi la Mama Samia UWT litakushika mkono kila hatua.”
Lazima tukaongeze idadi ya Viongozi wanawake kwenye mitaa na vijiji, UWT tukiongozwa na Rais wa kwanza Mwanamke Dkt. Samia Suluhu Hassan , tutahakikisha ushiriki wa wanawake kwenye chaguzi hususani kugombea utaongezeka, ufike mwisho wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na sio kuwapigia tu kura wanaume na katika hili kielelezo na kinara wetu ni Rais Dkt. Samia na ndio chachu ya mafanikio kwa wanawake.”Amesema Jokate.
Amesema Rais Samia ni msikivu, mvumilivu na anapenda kuona akina mama wanapata fursa na hawatakiwi kukatishana tamaa lazima waungane na kutiana moyo kwani Viongozi wengi wanapokuwa wanawake matokeo huonekana na takwimu zinaonesha akina mama ni viongozi bora.
Hata hivyo amewataka Wanawake wote kushirikiana kikamilifu na UWT ipo na kampeni mahususi ya kuhamisha wasichana na wanawake kujiuga na UWT kidijitali (kielekrtoniki), hivyo anawakaribisha kujiunga na jeshi la wapambanaji, wachapakazi na wapeana fursa na maendeleo.
“Dunia ya sasa imebadilika tunataka jeshi letu kulisoma kwenye kiganja, hivyo niielekeze UWT kwa Makatibu wote wa Wilaya ni kuhamasisha na kusajili wanawake wanachama wa UWT kwenye mfumo wa kidijitali.”
Amesema njia hiyo itasaidia katika kuwezeshana kiuchumi kwa kuwa itasaidia kujua idadi ya akina mama waliopo na hali zao na jinsi gani ya kuwasaidia mmoja mmoja au makundi.
Adha Jokate amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho siku ya mwanamke Dunia yatafanyika katika Mikoa yote ambapo Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda atakuwa mkoani Songwe Machi 8 na Machi 9 Jumamosi wataungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano mkoani Dodoma hivyo wanawake wajitokeze kwa wingi kwakuwa ni sehemu ya fursa na kuendelea kupeana elimu.

Hakuna maoni: