Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam.
WASANII wa Tasnia ya Filamu Tanzania (BONGO MOVIE) wamemshukuru na Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake ya kuanza kuwajumuisha Wasanii mbalimbali kwenye ziara zake rasmi nje ya Nchi kwa lengo la kujifunza zaidi.
Rais Samia alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa Albamu ya Staa wa Muziki wa Bongo Flava Hamarmonize aliyoiita "Muziki wa Mama".
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, 2024 jijini Dar es Salaam Muigizaji na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amesema kuwa jambo hilo ni kubwa na wanazo sababu za kumshukuru Rais Samia ambapo wao kama wasanii watahakikisha wanaitumia fursa hiyo katika kujifunza, kulinda maadili na kuitangaza Tanzania vizuri kiutamaduni na kiutalii jambo ambalo litaivuta Dunia kuifahamu vyema Tanzania.
Ameongeza kuwa Rais Samia anafanya hivyo kama mzazi anayepaswa kuwakumbatia watoto wake wote, ambapo ameleza kitendo cha Wasanii kupelekwa nje kujifunza kitawasaidia kuwainua kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma amesea kuwa kitendo hicho cha Rais Samia kinakwenda kuimarisha Tasnia ya Filamu Tanzania.
Hakuna maoni: