DMI NA GHANA WAANDAA KONGAMANO LA 3 UCHUMI WA BULUU.


Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Wadau wa wa sekta ya Bahari,utalii,uvuvi,mafuta na gesi wametakiwa kuhudhuria katika kongamano la tatu la uchumi wa bluu linalotarajiwa kufanyika kuanzia julai 4-5/2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) DKT. Tumaini Gurumo amesema kongamano hilo la Mwaka huu ni la kimataifa ambapo nchi zaidi ya 11 zitashiriki ikiwemo Ghana, Kenya, Comoro, Liberia, Nigeria, Sierra Leone, Denmark, Italy, Sweeden ,Korea Kusini, na China.

"Kongamano hili limeandaliwa na Chuo cha Bahari cha Dar es salaam kwa kushirikiana na Chuo cha Bahari cha Ghana".

Ameongeza kuwa ushiriki wa nchi mbalimbali unatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kukuza ujuzi katika matumizi ya vyanzo vya maji kwa maendeleo ya nchi na Afrika kwa ujumla.


Aidha amebainisha lengo kuu la kongamano hilo kuwa ni kuangalia fursa zilizopo kwenye maji namna vinavyotumika na kuongeza wigo wa fursa za kutumia vyanzo hivyo.

"Tunataka kutoka kwenye uvuvi wa mitumbwi na kuvua samaki wadogo tuanataka kwenda kuvua katika mwa. Bahari na kuvua samaki wengi zaidi,

Eneo lingine ukiacha uvuvi ni uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo shehena kubwa ya gesi na mafuta ipo kwenye bahari ambapo eneo hili bado halijafanyiwakazi vizuri ambapo tunatakiwa kuliangalia eneo hili kwa namna ya kipekee na kuongeza kasi.

"Wenzetu nchi nyingine wameshaanza kuchimba mpaka madini kwenye bahari na sisi tunapaswa kwenda huko".

Kongamano hilo linataongozwa na kaulimbiu isemayo "Kuiendea kesho:kujumuisha ulinzi na usalama wa majini, mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo ya teknolojia kwa ukuaji wa uchumi wa bluu"

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.