Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam siku ya Mei 21, 2024 maeneo ya Kipunguni B, Ukonga lifanikiwa kumkamata Hassan Yahya (Cobra) na wenzake watatu wakitumia dawa za kulevya aina ya bangi huku wakipanga njama za kufanya vitendo vya kihalifu yakiwemo makosa ya unyang’anyi kwa kutumia Silaha bandia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 7, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao walikutwa na pistol toy 7, AK47 toy 2, Jambia toy 2 na shoka toy 2, kama sehemu ya maandalizi ya kufanya kuhalifu.
"Jumla ya watuhumiwa 13 wanao husika na kuuza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya ikiwemo bangi walikamatwa ikiwa ni pamoja na Hamis Seif (18) Mkazi wa Mbondole na Bosco Bosco (18) Mkazi wa KipunguniIlala,".
"Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika kuzuia matukio ya kihalifu kwa kuafutilia kwa karibu makundi yote ya watu na hasa wanatumia dawa za kulevya na kufanya matukio ya kihalifu," Amesema Kamanda Murilo.
Ameongeza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa na Puli 531na kete 2,639 na misokoto158 ambayo ilikuwa tayari kutumiwa wakiwa pia na viroba vinne vya bangi pia pikipiki mbili MC 673 CKM na MC 591 CUW zilizokuwa zinatumika kusambaza bangi hizo pia zimekamatwa.
Akizungumzia kwa upande wa usalama wa barabarani amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
linaendelea kuwafuatilia, kuwakamata na kuwafikishwa mahakamani madereva wasiotii sheria na kanuni za usalama barabarani wakiwemo walevi na makosa hatarishi ya wapanda pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.
Jumla ya makosa 67 ya pikipiki yalikamatwa yakihusisha kutokuwa na leseni, kuzidisha abiria na kuendesha pikipiki wakiwa wamelewa ambapo madereva 21 walifikishwa mahakamani, na wengine walitozwa faini za papo hapo.
Amebainisha kuwa Madereva wa magari 6 walikamatwa kwa makosa ya kuendesha wakiwa wamelewa ambapo madereva wawili walifikishwa mahakamani na wengine 4 walitozwa faini papo hapo.
Vilevile katikakipindi chamwezi Aprili hadi Mei 2024, amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kusimamia mifumo ya haki jinai lilifanikiwa kupata matokeo Mahakamani ya watuhumiwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Agustino Daniel (22) Mkazi wa Vingunguti ambaye alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti kwenye Mahakama ya Wilaya Kinyerezi.
Wengine ni Conradi Nnkuru (43) mkazi wa Msongola kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kinyerezi alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa 3 kwenye Mahakama ya Wilaya Temeke walipata adhabu ya kifungo miaka 30 jela akiwemo Mikidadi Juma (40) mkazi wa Mbagala.
Hakuna maoni: