Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Vijana wa Dini zote wamehimizwa kushiriki katika tamasha la Twen'zetu kwa Yesu linalotarajiwa kufanyika Juni 15/2024 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam.
Mastai ameongeza kuwa vijana watakaohudhuria katika tamasha hilo hawatatoka kama walivyoingia kwani watapokea ujumbe wa neno la Mungu ambalo litatoa fursa kwa vijana kuenenda katika njia ifaayo.
Pia amesema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kuwabadilisha vijana kuwa na mtazamo chanya katika kumjua Mungu, Katika uchumi na uzalendo kwa Taifa lao pia wanawasisitiza wazazi na walezi kuendelea kuwaunga mkono vijana wote kushiriki tamasha hilo.
Mchungaji Mastai ameendelea kwa kubainisha kuwa tamasha hilo ni la 11 tokea lilipoanzishwa mwaka 2014 na limeendelea kukua kila mwaka ambapo kwa mwaka huu wanatarajia litahudhuriwa na vijana zaidi ya vijana Elf u 30,000.
Aidha tamasha litapambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mahubiri kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Syprian Yohana Hilint huku waimbaji wakiwa ni Rose Mhando,Neema Gospel Choir,Agape Gospel Band,Franc Jamrack, Boaz Danken,Kibonge wa Yesu,Hype Squad,Kariakoo KKKT Praise Team na kwaya ya sita zinazounda majimbo sita ya KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Kiingilia katika tamasha hili ni Tsh 5,000/= huku T-shirt ikipatikana kwa Tsh 20,000/=.
Aidha pia kwa mwaka huu tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga na litaendelea kupelekwa katika mikoa mbalimbali kila mwaka.
"Mkoani shinyanga tamasha la Twen'zetu kwa yesu litafanyika Agosti 10 katika uwanja wa kambarage ambapo hii ni mara ya kwanza kwa tamsaha hili kufanyika katika mikoa hiyo na mambo yakiwa mazuri zaidi mwakani tutaongesa mikoa mingine".
Hakuna maoni: