DAR ES SALAAM.
Viongozi wa Dini nchini wameitaka Serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa X ambao hapo awali ulikuwa unajulikana kama Twitter kutoka na kuruhusu maudhui ya video za ngono hususani za mapenzi jinsia moja yani Ushoga.
Wito huo wameutoa leo tarehe 11/06/2024 Jijini Dar es salaam wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari ambapo wamesema Mungu anachukizwa na vitendo viovu ikiwemo ushoga hivyo wamesisitiza Serikali kupitia mamlaka zake mbalimbali kuona haja ya kuudhibiti mapema mtandao huo ili kutoaribu maadili kwa vijana na watoto wa Kitanzania ambao ndio Taifa la kesho.
"Mungu yupo na tunapaswa kutende yanayompendeza, Mungu ameweka njia za asili za kushiriki mapenzi na si kinyume na maumbile kufanya hivyo ni kumchukiza Mungu".
"Tunafanya haya yote kwa manufaa ya Taifa letu,kwani Mungu akitaka kuangamiza Taifa hatachagua huyu alifanya au huyu hakufanya, kwahiyonili tusiendelee kumchukiza viongozi wadini tumeona tutumie fursa kuonya mwelekeo wa utandawazi nchini kwetu".
"Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe"
Ameongeza kuwa walimu wanashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na wanakutana na wanafunzi ambao tayari Wana viashiria vya tatizo hilo na wanapohoji wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao,hivyo ametoa wito kwa jamii nzima kuungana kupaza sauti kwa wanaoleta agenda za ushoga kupingwa vikali mara moja ili vitendo hivyo visiharibu kizazi cha Taifa lijalo.
Hakuna maoni: