Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Vyombo vya Habari Nchini vimetakiwa kuandaa vipindi maalumu kuhusu uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuvipatia muda mahususi (Prime time) ili viweze kusikilizwa na wengi na kupata elimu mbalimbali juu ya uchaguzi kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura hadi siku ya kupiga kura.
Akizungumza mapema leo Juni 14/2024 Meneja huduma za utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka wakati akiwasilisha Mada kuhusu Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuelimisha Umma juu ya uchaguzi ikiwa leo ni siku ya pili ya mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura mkutano ulioratibiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Kisaka ameongeza kuwa vyombo vya habari vinaunganisha jamii katika matukio ya kitaifa na kimaendeleo"tufahamu kwamba tunawajibu wajibu mkubwa katika kuchochea maendeleo ya Taifa kwa kuelimisha jamii".
Ameongeza kuwa Sera ya Habari na utangazaji ya mwaka 2003 Inatambua sekta hii kuwa ni ya huduma ya jamii nchini na ni haki ya msingi kwa Mwananchi kupata habari kwa mujibu wa katiba, pia Duniani kote hutambulika hivyo.
Aidha amevitaja vyombo vya habari vyenye nguvu zaidi Duniani ambapo Redio inashika namba moja licha ya maendeleo ya teknolojia yaliyopo na hiyo inachangiwa na gharama nafuu ya upatikanaji wake ambapo 76% ya matangazo ya Redio za Fm huwafikia watu.
"Upekee wa redio ambao watu wanaupenda ni kuwa mtu anaweza kupata ujumbe(kusikiliza) huku akiendelea na kufanya shughuli zingine".
"Television pia inapendwa na watu wengi kwasababu unatizama na unasikiliza lakini ni Tv set ni gharama hivyo humilikiwa na watu wachache, watu wanaohudumiwa na Tv kwa njia ya Satellite (DTH) ni 100% na kwa njia ya miundombinu ya Ardhi (DTT) ni 56% na idadi ya watu wanaomiliki visimbuzi ni milion 3.8".Amesema Kisaki.
Pia amebainisha kuwa asilimia 33% ya watu hutumia mitandao ya kijamii na hupata taarifa huko ambapo Amebainisha watumiaji kulingana na mtandao ambapo Whatsapp inatumiwa na watu milion 9.9, Facebook million 8.1, Instagram milion 3.67, you tube milioni 2.9, Tiktok milioni 1.6, Twitter 0.78 M.
"Vyombo vya Habari ni nguzo muhimu sana ya mafanikio katika mchakato mzima wa kuelekea uchaguzi" Amesema Kisaki.
Hakuna maoni: