DAR ES SALAAM.
JUMUIYA ya wafanyabiashira Kariakoo wamemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwawekea mazingira wezeshi ya ufanyabiashara ikiwemo namna ya utoaji mizigo bandarini.
Ameongeza kuwa katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu kijaji aliwaahidi wafanyabiashira kuongeza bajeti ya wizara kwaajili ya kuboresha mazingira ya biashara,kuwakutanisha na TRA na kuweza kuangalia namna ya kupunguza utitiri wa kodi.
" Tumewaomba TRA wanapotekeleza majukumu yao wasijifiche,tushirikisha e ,tufanyekazi kwa pamoja tujenge nchi yetu sote, wafanyabiashira tupo tayari kulipa kodi bila shuruti, Nipende kutoa wito kwa TRA hata wanapoleta vijana wapya katika kukusanyakodi watutambulishe wasinifiche wakawa wanawawinda wafanyabiashira".
Aidha amebainisha baadhi ya Kero zinazoendelea wakabili wafanyabiashira hao kuwa ni pamoja na VAT,namna ya uwasilishaji wa risit za EFD, na uingizaji wa mizigo kutoka nje.
Wafanyabiashira wanaomba kodi zote ziishie bandarini na si kuwafwata mara kwa mara katika maeneo yao ya biashara ili kuepusha mianya ya rushwa.
Peter hedson katibu ameiomba Serikali kuendelea kuwa na ushirikishwa katika shughuli mbalimbali pia hivinkaribu juni 13/2024 watakuwa na mkutano mkuu wa wafanyabiashira lengo likiwa kueleza mafanikio waliyoyapata na yale yote yaliyotekelezwa na Serikali.
Hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashira wote kujitokeza siku hiyo katika ukumbi wa Anatogol uliyopo ilala Jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni: