BODI YA SUKARI YATOA UFAFANUZI JUU VIBALI VYA UAGIZAJI SUKARI NJE YA NCHI YASISITIZA KUWA LENGO LAO NI KULINDA MASLAI YA WANANCHI.

Na Mwandishi wetu,

Dar es salaam.

BODI ya Sukari nchini imetoa ufafanuzi juu ya sakata la sukari nchini na kusisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kulinda maslai ya wananchi, wakulima, wawekezaji na wadau wengine muhimu kwa kuhakikisha inafanya maboresho makubwa kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam mapema hii leo Julai 05/2024 Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania Profesa Kenneth Bengesi,ikiwa ni siku chache baada ya kupitishwa sheria mpya ya sukari nchini amesema bado waneaendelea na majadiliano na wadau ili kutatua changamoto zote sambamba na kuikuza sekta ya sukari kwa sababu ni jambo nyeti na muhimu, hivyo wanalichukulia swala hilo kwa umakini.

Ameongeza kuwa sekta hiyo itafanya vema na kupata mafanikio zaidi kupitia majadiliano mbalimbali na wadau kwa maana jambo hilo ni nyeti na muhimu hivyo wanalichukulia kwa umakini kwa umakini mkubwa.

Siku chache zilizopita kumekuwa na mjadala mkubwa ndani ya Bunge na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu nchini kuhusu mikataba kadhaa iliyodaiwa kusababisha uhaba wa sukari nchini, ingawa ufafanuzi ambao umetolewa umeweka hali shwari.

Amefafanua kuwa wakati walipaoamua kulegeza mchakato wa uingizwaji wa sukari ilisababisha kuwepo kwa kiasi kikubwa kinachoingizwa nchini na kuyumbisha soko la ndani, hali iliyofanya Serikali kubadilisha Sheria na kubadili mfumo wa uingizaji wa bidhaa hiyo nchini jambo ambalo limesaidia kulinda soko la ndani.

Prof. Kenneth Bengesi ameeleza kuwa Sheria ya Usalama wa Chakula ilitumika kuingiza Sukari ya Dharura baada ya makampuni (Wazalishaji wa Sukari) kupewa vibali vya kuingiza tani (50,000) na kuishia kuingiza tani elfu sita (6,000) pekee tofauti na vibali vilivyowaelekeza jambo lililopelekea kutokea upungufu wa sukari na bei kuwa juu”

Ameongeza kuwa Vibali vya kuingiza Sukari nchini vilitolewa mapema kama kawaida lakini baadhi ya Wazalishaji wa Sukari (kampuni nne) ukiondoa ‘Kilombero Sugar’ walioingiza kiasi kidogo’, wengine hawakuingiza Sukari hata tani moja nchini, hali iliyopelekea upungufu na matokeo yake bei ya Sukari ikawa juu.

Baadhi ya watu wanaoelezea suala la sukari hawana taarifa za kutosha, hivyo ni jukumu letu Bodi kutoka hadharani pamoja na mambo mengine, kutoa picha kamili ya namna gani Watanzania wanaenda kupata ahueni kubwa baada ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria ya sukari nchini,”Alisema Profesa Bengesi.

Baadhi ya hoja zilizofafanuliwa na Bodi ya Sukari Tanzania ilikumbwa na uhaba wa sukari, malalamiko ya utoaji wa vibali na mbinu zinazoenda kutumika kwa lengo la kuhakikisha bidhaa hiyo kuwa adimu nchini inaenda kuwa historia.

“Mnajuwa dharura tuliyokuwa nayo, tulikuwa kwenye mazingira ya dharura kubwa na ilikuwa ni lazima tuchukue hatua ya dharura kukabiliana na tatizo lililokuwa mbele yetu, unapokuwa katika hali hii hautumii njia za kawaida, yaani nyumba inawaka moto upo ndani afu unatafuta mlango,? unachotafuta namna ya kutoka, kwahiyo sisi tuliangalia mbadala bila kuvunja taratibu” Prof. Kenneth Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari na kuendelea kwa kusema kuwa

“Tangu tulivyo binafsisha hadi sasa uzalishaji bado haujatosheleza mahitaji ya nchi, hivyo pengo la uzalishaji bado lipo na mfumo uliokuwa ukitumika miaka ya nyuma kuingiza sukari ya kuziba pengo tulikuwa tukitumia wafanyabiashara, lakini kwa sababu ilionekana kwamba sukari iliyokuwa ikiingia nchini ilikuwa ni kiasi kikubwa ambacho kilikuwa kikivuruga utulivu wa soko la ndani. Ilipofika mwaka 2015 serikali ilichukua jukumu la kufanya mabadiliko ya kanuni za sheria ya sukari za mwaka 2010 na kubadilisha mfumo wa uingizaji wa sukari” Prof. Kenneth Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari.



Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.