Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam.
Kamati ya Rufaa ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) imesema hivi karibuni ndani ya siku tano zijazo kutokea leoJulai 8/2024 kitatoa majibu ya rufani ya mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Bw. Doyo Hassan Doyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa Said Miraji amesema rufaa ni haki ya kila mwenye malalamiko kwa mujibu wa kanuni za Chama hivyo baada ya uchaguzi Mkuu wa ADC ambao Shaaban Haji Itutu alitangazwa mshindi Kwa kura 121 dhidi ya kura 70 za mpinzani wake Doyo Hassan Doyo hivyo Doyo kutumia haki yake ya msingi kukata rufaa.
Ameongeza kuwa hoja saba zilizotolewa na Doyo kwenye kamati hiyo ambazo ni pamoja na Mwenyekiti aliyekuwa Madarakani kuendelea na uenyekiti wa kikao hadi mwisho wa mkutano ikiwa ni kinyume na Katiba na kanuni za ADC, ongezeko la wapiga kura, kuzuiwa kufanyika kwa Kampeni na mkutano kutokufata Sheria ya vyama vya siasa.
“Rufaa ni haki ya kila mwanachama kwa mujibu wa katiba kati uchaguzi pia Katiba ya ADC inaruhusu wataalamu kuruhusiwa kuingia katika kamati kupitia kifungu cha 12 cha katiba hiyo” Amesema.
Hata hivyo amesema Kamati iliwasilisha barua kwa upande wa walalamikiwa ambapo nao waliwasilisha pingamizi na kudai kuwa Doyo anafanyavikao na waandishi bila kusikiliza maamuzi ya kamati.
Ameongeza kuwa walikutana na pande zote mbili na kufanya upatanisho kwanza na baadae kuendelea na kikao na kukubaliana kwamba wataendelea kulitatua swala hilo ndani ya chama na ambaye hataridhika na maamuzi ya ADC basi ataruhusiwa kuendelea kutafuta haki katika ngazi zinazofwata.
“Upatanisho na suluhu huleta umoja,amani na mshikamano katika taifa na jamii kwa pamoja hivyo maridhiano hayo yametoka na misingi sita ikiwemo katiba ya ADC, Amesisitiza na kuongeza kuwa,
“Tumeona maridhiano yanapokosekana huleta mfarakano ndani ya chama,na tumeona katika vyama vya upinzani kila baada ya uchaguzi panatokea mtafaruko mfano katika vyama mbalimbali wakifarakana kwa kukosa maridhiano,tumeona katika chama cha CUF, CHADEMA wanachama wanahama na kwenda vyama vingine”
Hata hivyo ameongeza kuwa ndani ya siku tano wanatarajia kuwa wamemaliza swala hilo,na kusisitiza kuwa wote ni wanachama wa ADC na mtafaruko huo ni chachu ya kukua kwa demokrasia.
Ametoa wito kwa vyama vingine kuunda kamati za rufaa na maridhiano zinazohusisha watu kutoka nje ya chama ili kuhakikisha kunakuwa na demokrasia ya kutosha katika maamuzi yote yanayofanyika.
Hakuna maoni: