KAMPENI YA FURSA KWA VIJANA YAZINDULIWA DAR IKIJUKIKANA KAMA "TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA KIJANI CAMPAIGN".




Dar es salaam.

VIJANA nchini wametakiwakujitokeza Kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Vitongoji utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Wito huo  ameutoa leo, Julai 6, 2024 Mjumbe wa NEC, Idara ya Organization wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Issa Gavu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wakati, akizungumza na vijana mbalimbali wakati akizindua kampeni kwa vijana kutumia fursa zilizopo ambazo zimetengenezwa na Serikali ya awamu ya Sita ili kujikwamua kiuchumi.

 "Nawaomba vijana ambao mmejitokeza hapa kwa wingi kwa hakika mmetuheshimisha na wale mnaotusikiliza na kutuangalia kupitia mitandao ya kijamii mjitokeze kugombea kushiriki kikamilifu kwenye siasa na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kulijenga taifa imara lenye viongozi bora.

" Leo tunazindua Kampeni ya Tunazima Zoote, Tutawasha Kijani kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM ) lengo ni kuhamasisha vijana kujiandaa na uchaguzi na mjiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hivyo nawaomba tuwe wamoja kupitia UVCCM ili tufanikiwe pamoja na kuipeperusha vema bendera ya CCM, kwani nyingi ndio ngumu muhimu katika uhai wa chama chetu," amesema

Gavu katika mkuatano huo alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwanadiplomasia Dk. Emmanuel Nchimbi , amesema chama hicho kinawapa fursa vijana ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Kwa maana, Tanzania ya leo na ya kesho inaundwa na vijana na endapo watatumia vizuri nafasi watakazozipata ni vizuri kuendeleza amani, imoja na mshikamano uliopo nchini.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.