Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.
Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kata ya Pugu Stesheni Jimbo la Ukonga
Wilaya ya Ilala Shaaban Mussa mwisho wa wiki tarehe 19/07/2024 alifanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo.
Katika mkutano huo uliokuwa na agenda ya uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kipindi cha kuanzia Januari hadi June 2024.
"Nilikiwa nimejipanga vilivyo kuja kuzungumzia masuala ya maendeleo na wananchi iliwaweza kujua utekelezaji wa Ilani yetu ya CCM kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo nimeweza kushirikisha idara zote katika masuala ya elimu msingi pamoja na elimu sekondari,"amesema Mussa.
Amesema kuwa sekta zingine pia kama ulinzi ,afya wadau wote hao niliwaita kufika na wameeleza yote yaliyo fanyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya hiyo ,Alhaj Said Sultan Sidde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara wa kata ya kata hiyo amesema amempongeza Mh. diwani kutimiza matakwa ya katiba ya nchi na chama cha mapinduzi kuandaa mkutano ili kutoa fursa kwa wananchi kufahamu maendeleo yao na mipango ya serikali.
Aidha Mwenyekiti alimpongeza Mh .Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo katika wilaya yote ikiwemo kata ya Pugu "Station".
Mwenyekiti pia alimpongeza Mh .Jerry Silaa Mbunge wa Ukonga na waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi kwa namna anavyopambania wananchi wa Ukonga kuwaletea maendeleo.
Sidde alihaidi kwa wananchi wa kata hiyo kuhakikisha ahadi zilizohaidiwa wakati wa kuomba kura 2019/2020 zinatekelezwa ipasavyo.
Aidha Mwenyekiti alihaidi kuziwasilisha kwa mkurugenzi wa jiji changamoto zote zilizowasilishwa ikiwa pamoja na uhaba matundu ya vyoo,maktaba,uwanja wa michezo,vitendea kazi kwa polisi jamii.
Mwenyekiti alipongeza namna ya uwasilishaji wa ilani ulivyofanyika kwa watumishi wa serikali kisekta kupanda jukwaani kuelezea mambo yaliyofanywa na serikali kwa kutaja fedha zilizopokelewa .
Mwenyekiti alieleza utaratibu huo unapaswa uigwe na kata nyingine kwa kuwa pia inatoa fursa kwa wananchi kuwafahamu watendaji wa serikali kwa mamlaka na idara zao .
Mwenyekiti wa wilaya pia aliwataka wananchi Pugu station kujiimarisha kiuchumi kutokana fursa kuwepo kwa kituo cha treni mwendokasi katika kata yao.
Mwenyekiti aliwataka wananchi kukiunga chama cha mapinduzi katika chaguzi zijazo kwa kuwachagua wagombea toka CCM.
Hakuna maoni: