SHIRIKA LA POSTA LAINGIA MKATABA NA AZAM PESA,LAPONGEZWA KWA JITIHADA ZAKE KATIKA KUJIIMARISHA.




 DAR ES SALAAM.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amelipongeza Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kutekeleza falsafa ya 4R za Rais Samia hasa ile ya Mabadiliko (Reforms) kwa ubunifu wa kuboresha utendaji wa Shirika hilo kwa kuingia mashirikiano ya kibiashara na Sekta binafsi.


Mhandisi Mahundi amezungumza hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye kuzindua na kushuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa kibiashara kati ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Azam Pesa iliyofanyika leo Julai 17, 2024,Jijini Dar es salaam.


Amesema kuwa ushirikiano baina ya TPC na Azam Pesa utaenda kuzinufaisha pande zote mbili za mashirikiano kwa kuongeza wigo wa wateja, kuongeza mapato na kuimarisha mzunguko wa kifedha kuanzia kwa mwananchi wa kawaida hadi mwenye kipato cha kati na cha juu kwa ajili ya urahisishaji wa shughuli za maendeleo ya mtu mmoja mmoja, na Taifa kwa ujumla.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.