Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Watumishi Housing Investiment (WHI) hii leo imeingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya kichina ya Shadong Hi-speed Group kwaajili ya ujenzi wa Nyumba 101 katika eneo la Mikocheni Really Estate Jijini Dar es salaam.
Akizingumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiment DKT Fred Msemwa amesema ujenzi huo unatarajiwa kuanza mapema Mwezi Agosti 2024 ambapo watajenga jengo lenye ghorofa 12 likijumuisha Nyumba 101.
Ameongeza kuwa Ujenzi wa Mradi huo unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 18.6 huku ujenzi wake ukifanyika kwa kipindi cha miezi 18 , na uuzaji wake ukiwa ni maalumu na nafuu kwa watumishi wa umma pekee.
"Chumba kimoja chenye sebule,chumba cha kulala, choo, stoo, jiko, balcony itaanzia Shilingi Milioni 99 na bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala itaanzia Shilingi Milioni 234/= " amesema Dkt. Fred na kuongeza kuwa
"Bei hizi zinaonekana ni za juu ukilinganisha na tulizouza hapo nyuma hii ni kutokana na kupanda kwa grama mbalimbali ikiwemo kupanda kwa vifaa vya ujenzi na Dola. Bei za nyumba hizi zikilinganishwa na nyumba za aina hii katika eneo la Mikocheni, nyumba hizi ni nafuu kwa kati ya asilimia 10% hadi 40%".
Pia Dkt. Msemwa Amesema kuwa uuzaji wa nyumba hizo tayari umeanza na wanatarajia mwitikio mkubwa kutoka kwa warumishi wa umma huku akisistiza kuwa mradi huo unalenga kuwapatia watumishi fursa ya kumiliki makazi yenye thamani na ubora wa hali ya juu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ushauri na ubunifu Arch Sephania solomon amesema ujenzi huo ni wakisasa na WHI imesanifu majengo hayo ya grorofa 12 wenyewe ambapo yamezingatia viwango vya ubora vya mikataifa huku yakiwa na mifumo ya ICT ambapo itawawezesha wakaazi kupata huduma kimtandao kirahisi.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi-speed Group Li Manchao ameaihidi kujenga majengo hayo kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati na kuhakikisha wanakata kiu ya WHI na kuongeza uaminifu kwa jamii.
Pia amewashukuru WHI kwa kuwaamini na kuwapatia mradi huo na kusema kuwa wanauzoefu wa kutosha katika ujenzi wa majengo kimataifa.
Aidha Watumishi Housing Investiment imeshajenga jumla ya nyumba 1,003 katika mikoa 19 nchi nzima Tanzania ambapo Nyumba 101 zinazokwenda kujengwa ni sehemu ya nyumba 218 zitakazojengwa katika mikoa ya Dodoma, Singida, Pwani, Ruvuma katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Hakuna maoni: