Na Mwandishi Wetu,
Dodoma.
WAKULIMA na wafugaji nchini wameshauriwa kutumia bidhaa za Kampuni ya AFRICAB kwa kuwa zina ubora unaotambulika kimataifa.
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Masoko wa Kampuni ya AFRICAB, Khalid Said wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, kwenye viwanja vya Nananane Nzuguni mkoani Dodoma.
Amesema kampuni hiyo inajihusisha na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za umeme zilizothibitishwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na nje ya nchi, hivyo kuwataka Watanzania hasa wakulima kuzitumia kwa kuwa ni bora na salama.
Khalid amesema AFRICAB ina bidhaa za kilimo kama mashine ya kuvuta maji (Water Pump za 0.75 HP hadi 2HP), submissible wire, drill aerth agger ambayo inaweza kuchimba ardhi urefu wa futi mbili na nusu kwa kutumia mafuta lita moja na nusu, huku ikifanya kazi katika viwango bora.
Mratibu huyo amesema mashine hizo zina ubora mkubwa, hivyo kuwataka wakulima kufika katika maonesho ya nanenane ili kupata elimu zaidi.
“Tumekuja na vifaa vya kisasa ambavyo vinaenda kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo. Rai yangu ni kwa wakulima na wafugaji kununua kwani watakuwa wamechagua kilicho bora,” amesema.
Aidha, amesema kampuni yao inazalisha na kusambaza aina mbalimbali za waya kama Kilamanjaro Cable, PVC, hose pipe zenye ukubwa kuanzia mita 25 na hadi 100.
Khalid amesema pia wanazalisha na kusambaza taa ambazo zinaweza kutumia na wakulima na wafugaji, hali ambayo inaonesha dhamira yao ya kuwezesha Watanzania kutumia bidhaa za ndani.
“Sisi AFRICAB tunajisifia kwa bidhaa zetu kuwa na ubora, lakini pia bei yake ni nzuri, hivyo tunawaomba wakulima, wafugaji na watanzania kununua bidhaa za ndani,” amesema.
Amesema kuna PVC za aina zote, waya, kebo, transfoma, kopa, condit, na zingine zinazalishwa hapa nchini.
Khalid amesema AFRICAB inazalisha bidhaa ambazo zinamlenga kila Mtanzania akiwemo wa hali ya chini, kati na juu.
Mtaribu huyo amesema tangu waanze kuzalisha na kusambaza bidhaa za kilimo na ufugaji wamepata mwitikio mkubwa, jambo ambalo linatoa mwanga mzuri.
Khalid amesema makao makuu ya AFRICAB yapo ina Mkoa wa Dar es Salaam na kuna matawi Dodoma, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya.
Hakuna maoni: