Dar es salaam.
Kampuni ya A2V Television Studio, imeandaa tuzo za filamu za kiswahili Afrika, lengo kuu ni kukuza kiswahili kupitia vipindi vya television, filamu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki hasa zile zisizozungumza lugha ya Kiswahili.
Mchakato mzima wa ukuzaji kiswahili, filamu na utoaji wa tuzo utasimamiwa na Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la taifa na bodi ya filamu Tanzania.
Tamasha limepewa jina la International Film Festival Afrika Award 2024,2025 ambapo uzinduzi wake ulifanyika Julai 7, 2024 jijini Dar es Salaam na kutamatika kwa mashindano ni Novembe 28, 2025 Kigali nchini Rwanda, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Bi Jannette Kagame.
Akizungumza hayo leo Agosti 6, 2024 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Baraka Chigele, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya A2V Television Studio.
"Tamasha litafanyika nchini Rwanda huku likihusisha nchi zote za Afrika ambazo zipo tayari kuleta filamu zao za kiswahili kuingia kwenye mashindano, lakini pia hata zile zilizopo nje ya Afrika zinaruhusiwa ili mladi tu ziwe zimetumia lughaya Kiswahili hata kwaudogo", amesema Chigele
Mpaka sasa nchi 16 kutoka Afrika zimekubali kushiriki mashindano hayo, na nchi 2 kutoka nje ya Afrika ambazo ni Canada na Ujerumani.
Kwa upande wake Jamal Mbaga ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mashindano hayo, amesema sababu ya kuanzishwa mashindano hayo, kiswahili kwa sasa ni lugha ya kimataifa hivyo kuna haja ya kukitanua zaidi.
"Katika lugha 10 zinazokua kwa kasi hapa Afrika lugha ya Kiswahili inaongoza hivyo kuna kila haja ya kukieneza zaidi na sisi tunataka kukieneza kupitia filamu za kiswahili kutoka Tanzania", amesema Jamal
Ameongezea kusema kwamba ni muda sasa wasanii wa filamu kutoka Tanzania kutengeneza kazi nzuri na zenye ubora ili kushindanishwa na wasanii wengine wa filamu Duniani kote.
Wasanii wa filamu kutoka Tanzania wanaombwa kupelekea kazi zao kwenye mashindano bila ya kuogopa kwani hii ni mara ya kwanza kuanzishwa mashindano hayo, huku ikielezwa kwamba majaji watakaotoa maamuzi hawatakua na upendeleo wowote.
Hidaya Njaidi ambaye ni barozi wa mashindano hayo akisisitiza wasanii wa kuigiza waende shule wasome juu ya kile wanachokifanya.
"Kwani vyuo mbalimbali vipo tayari kupokea wasanii wa maigizo ili iwasaidie kuandaa kazi zenu kwa mashindano ya kimataifa" amesema Hidaya
Wasanii wa maigizo wanaombwa kutumia vizuri hii nafasi kwani ni miongoni mwa sababu itakayosaidia kupelekea kazi zao kimataifa ambapo ni miongoni mwao.
Hakuna maoni: