CHEKA TU YAPANIA KUKUSANYA WATU 10,000 LEADERS CLUB OKTOBA 5, 2024.

 


DAR ES SALAAM.

Tamasha la uchekeshaji linalojulikana kama "Cheka Tu" linalosimamiwa na Clouds TV linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam tarehe 5 Oktoba 2024. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Cheka Tu, Conard Kennedy, alieleza kwamba uchekeshaji ni biashara na ajira muhimu kwa vijana wengi wa Kitanzania, ambao wamejiajiri kupitia sanaa hii. Alisema kuwa jukwaa la Cheka Tu msimu wa pili litafanyika katika viwanja vya Leaders Club huku kiingilio kikianza shilingi 15,000, 30,000 na 50,000, na lengo ni kuwapa fursa Watanzania wengi kushiriki na kufurahia tamasha hili.


Kennedy alifafanua kwamba tamasha hili linatarajiwa kuvutia zaidi ya watu 10,000, kutoa fursa kwa Watanzania kuona ukubwa wa komedi nchini.


Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mikakati na Ubunifu wa Clouds Media Group, Reuben Ndege, alisisitiza kuwa Cheka Tu imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa vijana wengi, ambao wameweza kujituma na kutimiza malengo yao kupitia vipaji vyao.




Mchekeshaji maarufu, Conchester Koku, anayejulikana kama Mama Mawigi, aliongeza kuwa amejipanga kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji. Akizungumza na waandishi wa habari, Mama Mawigi alisema atatumia uzoefu wake wa miaka saba kuwaburudisha na kuwaelimisha Watanzania. Aliahidi kwamba tamasha hili litakuwa la kihistoria, likijaa furaha na kicheko kutoka kwa wachekeshaji wote.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.