MAPITO FOUNDATION WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI WAFANYAKAZI WANAONYANYASWA UGHAIBUNI.

 


Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Mapito foundation waiomba Serikali kuingilia kati unyanyasi wa wa wasichana wa kazi wanaosafirishwa kwenye mataifa mengine kwa kuhakikisha mabinti hao wanarejeshwa nchini pamoja na kufuta usajili wa mawakala wasiofwata utaratibu.

Akizingumza na Waandishi wa Habari ofisini kwao leo September 05/2024 Jijini Dar es salaam Mtangazaji wa Global Tv Na Mkurugenzi Mtendaji wa Mapito Foundation Zalium Tabuyanjaa amesema kuwa Kutokana na matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani hususani katika nchi za kiarabu kuripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari Global Tv kupitia Kipindi cha mapito wameweza kufwatilia swala hilo na kuhoji wasichana kadhaa ambao wengi wao wanapitia mateso makubwa wakiwa ughaibuni.

Ameongeza kuwa baada ya mahojiano na waathirika wa matukio hayo wamebaini kuwa sababu kadhaa zinazowafanya wao kupitia katika changamoto hizo ikiwemo kudanganywa na watu mbalimbali kuwa huko watapa kazi za mishahara mizuri na maisha mazuri,kuwepo kwa mawakala feki wanaowaahidi kuwasafirisha na kiwasaidia pindi wapatapo changamoto,kutoroshwa kwa mabinti na kupelekwa nje ya nchi kwa njia za panya.

Hivyo kutokana na sababu hizo wanaiomba Serikali na Taasisi zake kufwatilia usajili wa mawakala wanaowasafirisha watu kufanyakazi nje ya nchi,kuboresha ulinzi katika mipaka ili kudhibiti utoroshwaji wa mabinti hao,kusimamia na kufuatilia na kuhoji wafanyakazi wanaoenda kufanyakazi nje ya nchi ili kujua maendeleo yao,kutoa elimu juu ya ajira za nje na utaratibu wa kwenda kufanyakazi huko,kuweka mawasiliano ambayo yatakuwa rahisi kwenye shida kupiga na kupata msaada akiwa nje ya nchi.

"Global Tv kupitia Kipindi chake cha mapito kimefanikiwa kumsaidia binti mmoja aliyekuwa amekwama Iraq ambaye amepitia mengi ambayo amezungumza kupitia Global Tv ikiwa kunyanyaswa, kuteswa,kupigwa na kuzuiwa kurudia nchini mpaka ambapo zilitumika nguvu za ziada mpaka kuhakikisha anarejea nchi,tunaishukuru Serikali kwa kutuunga mkono na tunaomba iweze kuongeza nguvu katika kuhakikisha inawasaidia waliokwama na wanaoendelea kurubuniwa wasiweze kufikia hatua mbaya zaidi".

Kwa upande Binti huyo Rahma Maneno ambaye amesaidiwa na Global Tv kurudi nchini kutoka Iraq alipokuwa anafanyakazi na kuteswa ambapo amesema Agent wake alipitia njianza panya kumfikisha huko na walifikia katika jumba kubwa ambalo lina mabinti tofauti tofauti ambapo kwenye jumba hilo mabosi wengi hufika na kuchukua binti wamtake kwaajili ya kuwafanyia kazi.

Ameongeza kuwa alifanikiwa kupata kazi na kupita kwa mabosi kadhaa ambapo kote alipitia manyanuaso makubwa ikiwemo kupigwa,kutemewa mate,kusemwa, kufanyishwa kazi kupita kiwango,kunyimwa chakula ikiwemo kufanyakazi kwenye nyumba mbili kila siku, pamoja na kufanyishwa kazi za kutweza utu.

Kupitia changamoto hizo amepatwa na shida ya afya ambapo amebainika kuwa na vitu kwenye Ubongo ambavyo vinapelekea kuwa na shida ya kumbukumbu ambapo husau vitu na yote hayo ya atoka na na vipigo alivyokuwa akipatiwa na wakati mwngine walikuwa wakimpiga mpaka kichwani.

Nae Suleiman Rashid ambaye ni wakala wa usafirishaji wafanyakazi nje ya nchi ambaye ameshirikiana na Global Tv kumrudisha binti huyo, Amesema utaratibu wa kusafirisha washichama wa kazi haujawekwa sawa,kunahitaji kuwekwa utaratibu mzuri ikiwemo mawakala kujijenga na kuwa uwezo wa kuwasaidia mabinti wanaopata changamoto mbalimbali.

Pia amewataka watu wanaotaka kwenda kufanyakazi nje ya nchi wanapaswa kutafuta mawakala waaminifu na kuchagua nchi ambazo hazina historia za kunyanyasa wasichana wa kazi.

Aidha Global Tv kupitia kipindi cha mapito wameahidi kuendelea kuwasaidia mabinti wengine waliokwama nje pia wapotaari kushirikiana na serikana taasisi mbalimbali katika kuhakikisha wanakomesha kadhia hiyo.



Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.