"Mkaa unapatikana kutokana na miti kukatwa, sasa ipo miti mingine ina sumu na mkaa unaweza ukawa umepatikana kutoka kwenye miti hiyo, hivyo kuathiri afya ya mtumiaji." Amesema Dkt. Gwajima
Amezitaja sumu zinazotokana na miti kuwa ni pamoja na carbon dioxide na carbon monoxide hivyo mtu anapovuta moshi unaotokana na kuni na mkaa, moshi huo huenda kwenye mapafu na kusababisha oxygen kwenye damu kupungua.
Kuhusu ladha ya chakula kupungua kutokana na kutumia nishati safi ya kupikia, Dkt. Gwajima amesema matumizi ya nishati safi katika kupikia hupelekea chakula kuwa kitamu na kisichokuwa na harufu ya moshi.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum ina vyuo nane vya Maendeleo ya Jamii ambapo viwiili tayari vinatumia nishati safi ya kupikia.
Hakuna maoni: