WAMACHINGA MKOA WA DAR ES SALAAM WAANZA MCHAKATO WA VITAMBULISHO, KUWEZESHA KUFIKIA TAASISI ZA KIFEDHA.

Published from Blogger Prime Android App
Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Anastaz Mpanju akizungumza jambo na Katibu wa Machinga Dar es salaam, Augustino Choga.Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Anastaz Mpanju

Na Mwandishi Wetu,

Dar es salaam.

Kufuatia taratibu mbali mbali za viongozi wa Chama Cha Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na maono makubwa ya kuwakwamua kufikia vipato vikubwa tayari viongozi hao wameweka Waziri kuwa ,wapo na serikali katika maono ya kuanza mchakato wa kujana vitambulisho vitavyoweza kuwa suluhisho hata kwenye taasisi mbali mbali mbali za kibenki.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Mkoa huo Agustino Choga alipo kuwa akizungumzia mtazamo mpya wa kibiashara katika ujasiriamali mdogo mdogo unaofanywa na wafanyabiasha hao .

"Tupo katika hatua nzuri ya maono ya kuja na vitambulisho vitakavyo leta chachu ya mafanikio juu yetu sisi wajasiriamali wadogo ambavyo vitakuwa na maitaji yote na kuwa vitasaidia kutambulika kwenye taasisi za kifedha nchini," amesema Choga.

Amesema kuwa hesabu zetu za kwanza ni wamachinga kumiliki nyumba ambapo ni mchakato unaoendelea kwa sasa kuna imani kubwa hatua hii itakuwa itakuwa imemalizika hivyo zoezi la kuja na vitambulisho litakuwa limeisha someka kama wamiliki wa nyumba na nyaraka zao zitakuwa zinaruhusu kukopesheka kwenye taasisi za kifedha.

Choga amepambanua kuwa kabla ya ujio huo wa vitambulisho wataanza kuwapatia elimu ikiwa itakayo saidia zoezi kufanyika kwa haraka.

Aidha kiongozi aliweza kukumbusha kuwa awali mchakato wa kumiliki nyumba ulisha anza Ambapo mbele ya waandishi wa Habari siku ya Mei 7,2024 wakati wa zoezi la utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa nyumba hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dkt Ibrahim Mwangalaba alisema Bank ilipokea maombi kutoka Wamachinga Dar es Salaam.

Mwangalaba alisema ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo walikubaliana kuanza ununuzi wa viwanja ambapo tayari wameshapata hekari 89 katika kijiji cha Magoza wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

"Licha ya kufanya ujasiriamali katika hatua zetu leo hii tumeweza kupata mikopo ya kimaendeleo hatua inayochangia kukuza uchumi wa mjasiriamali mmoja mmoja,"amesema Choga.

Maendeleo Banki kwa ushirikiano mzuri na wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam tayari wamekuwa chachu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kumkwamua mwananchi kiuchumi ili kupunguza umaskini ambapo walishaingiamakubaliano na chama cha wamachinga Kariakoo kwaajili ya kuwapa wamachinga mikopo ya gharama nafuu ya ununuzi wa viwanja pamoja na mkopo wa ujenzi wa nyumba za kisasa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.