
29 Novemba, 2024, Dar es Salaam.
Kamati ya Uongozi Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kikao cha dharura kilichofanyika jana, imetangaza msimamo wake kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Chama hicho kimesema kwamba uchaguzi huo haukuwa dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), bali ulikuwa uchaguzi dhidi ya dola na linataka uchaguzi huo ubatilishwe na kufanyika upya.Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Jonas Semu, alisema kwamba mchakato mzima wa uchaguzi, kuanzia hatua ya utungaji wa kanuni hadi utoaji wa matokeo, ulidhihirisha uvunjaji wa misingi ya haki na demokrasia. Alisema mamlaka ya kusimamia uchaguzi (TAMISEMI) ikisaidiwa na vyombo vya dola, vikiwemo vikosi vya ulinzi na usalama, vilihusika katika uharibifu wa uchaguzi kwa kuhusisha matukio ya vitisho, ukamataji wa raia, kutekwa kwa wanachama wa chama hicho na matumizi ya kura bandia.
"Taarifa kutoka maeneo mbalimbali, kama vile Manispaa ya Kigoma Ujiji, zimeonyesha kuwepo kwa matukio ya kura bandia, ambapo hata askari wa jeshi walikamatwa na wananchi wakiwa na mamia ya kura zilizokusudiwa kuingizwa kwenye sanduku la kura," alisema Semu.
Katika hatua nyingine, ACT Wazalendo imeitaka serikali na vyombo vya usalama kuwachilia haraka wanachama na viongozi wake zaidi ya 60 waliokamatwa kwa kudhibiti uhuni katika uchaguzi huo. Chama hicho kimesema kwamba kinaendelea na uchambuzi wa matukio ya uchaguzi na kitatangaza taarifa kamili kuhusu mwenendo wa uchaguzi huo.
ACT Wazalendo pia imesema kuwa itaendelea kufanya mawasiliano na vyama vya siasa na asasi za kiraia kwa lengo la kuunda mkabala wa pamoja utakaohakikisha mageuzi katika mifumo ya uchaguzi nchini, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Kat
Hakuna maoni: