KONGAMANO LA 14 LA TAASISI YA WAHANDISI KUFANA, WAZIRI MKUU MGENI RASMI.

Published from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), litakalofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Desemba mwaka huu, kwenye ukumbi wa kimataifa wa Arusha (AICC), Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa IET, Ipyana Moses, amesema kongamano hilo litawashirikisha wahandisi, mafundi, wanafunzi, na wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Aidha, Moses ameeleza kuwa washiriki zaidi ya elfu moja wanatarajiwa kushiriki huku baadhi wakiungana kwa njia ya mtandao, ambapo mafunzo mbalimbali kuhusu masuala ya uhandisi yatatolewa.

Dhima kuu ya kongamano hilo ni "Kuza na Fanya Ubunifu, Uhandisi Bora katika Dunia Inayobadilika." Mada zitakazowasilishwa zitajikita katika kutoa elimu bunifu na kuhamasisha ubunifu katika uhandisi, huku kongamano likilenga kuondoa dhana ya ufanyaji kazi wa kimazoea.

Moses ametoa wito kwa wahandisi na wadau wa sekta mbalimbali za uchumi nchini kushiriki katika kongamano hili, na kuwashauri wahandisi na mafundi ambao bado hawajaunga na IET kujitokeza na kujiunga na taasisi hiyo.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.