NLD KUTIKISA UBUNGO KESHO NOVEMBA 25, KWA KAMPENI KABAMBE.

Published from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Kesho, tarehe 25 Novemba, saa 10 jioni, viwanja vya Kwakomba, Mtaa wa King'ongo, Ubungo, Jijini Dar es Salaam, Chama cha NLD kitakuwa na mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mtaa.

Viongozi wa NLD wilaya ya Ubungo wanachukua fursa hii kuwakaribisha wananchi wote wa wilaya ya Ubungo kwenye mkutano huo wa kumnadi mgombea wa Chama cha NLD Mtaa wa King'ongo, Mhe. Patriki Hilaly Ngayungwa.

Mkutano huo utaudhuriwa na viongozi wa NLD kutoka makao makuu, kwa lengo la kuunga mkono na kutoa motisha kwa mgombea wa Chama hicho.

Chama cha NLD kinaendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni nchi nzima, huku viongozi wake wakisisitiza kusimamisha wagombea wenye ushawishi katika kila mtaa, kijiji, na kitongoji.

Uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, nchi nzima.

By Ombe B. Kilonzo

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.