NLD KUZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KESHO MKOANI TANGA.

Published from Blogger Prime Android App

Na Ombeni B.Kilonzo.

Chama cha National League for Democracy (NLD) kinatarajia kuzindua rasmi kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji kesho, Novemba 20, 2024.

Uzinduzi huo utafanyika katika Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ambapo viongozi mbalimbali wa chama hicho watashiriki.

Kampeni zitakazozinduliwa katika kijiji cha Kwedkwazu Mashariki, zitaendelea kuhamasisha wanachama na wananchi katika maeneo mengine ya Tanga na mikoa mingine ya nchi.

Katibu Mkuu wa NLD, Doyo Hassan Doyo, amesisitiza kuwa baada ya uzinduzi, kampeni za chama hicho zitafanyika nchi nzima, hasa katika maeneo ambapo NLD imewasimamisha wagombea.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.