RUVUMA.
TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma yaokoa fedha zaidi ya Milioni 16,736,800/- kwa kudhibiti vitendo vya rushwa na kuwafikisha mahakamani washtakiwa mbalimbali.Miongoni mwa washtakiwa waliofikishwa Mahakamani ni Viongozi wa Majimaji Amcos Tunduru na Mzabuni aliyesambaza vifaa vya Ujenzi Hospitali ya Wilaya ya Madaba ambapo Washtakiwa walitiwa hatiani na Mahakama imewahukumu kulipa faini pamoja na vifungo.
Hayo yamesemwa na Bi. Janeth Francis Haule Naibu Mkuu wa TAKUKURU (M) Ruvuma, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mkoa wake kwa kipindi cha mwezi Julai - Septemba 2024.
Hakuna maoni: