

DAR ES SALAAM.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu akiwahutubia wananchi wa Mtaa wa Nyambwela, Jimbo la Temeke, amesema kuwa Chama hicho kinaziunga mkono kauli za Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristu (CCT) kuupinga uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
"Tupo pamoja na Maaskofu kwenye hili. Wamesema ukweli wa Mungu. Sote inabidi tupaze sauti zetu kupinga uhuni uliofanyika kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Ule haukuwa uchaguzi bali ni uchafuzi"-alisisitiza Ado
Hakuna maoni: