Na Mariam Muhando,
Dar es salaam.
Katika kuhakikisha Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam inakabiliana na changamoto ya mrundikano wa Watoto Mashuleni inatarajia kuzindua Shule ya Sekondari Amani itakayokuwa na uwezo wa kupunguza Wanafunzi Zaidi ya 900.
Akizungumza Jijini hapa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Muheshmiwa Edward Mpogolo mara baada ya kufanya ziara yenye lengo la kukagua Maendeleo ya miundombinu ya Elimu ili kuwapokea Wanafunzi wa Awali, Darasa la kwanza na Kidato Cha kwanza kuelekea January 2025.
Mpogolo amesema dhamira ya Jiji la Dar es salaam ni kuhakikisha Wanafunzi wote wanapata nafasi ya kuingia Darasani hivyo Watoto zaidi ya elfu 41 wataingia Shule ya Msingi na elfu 34 wamefaulu Kidato Cha kwanza.
"Tunamshukuru Muheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ukarabati wa madarasa na Ujenzi wa Shule mpya ili Watoto waweze kupata Elimu Bora",Alisema Mpogolo.
Wakati huo huo amewataka Wakandarasi kuhakikisha wanafanyakazi saa 24 na kukamilisha Miradi Kwa wakati ili Watoto waweze kuingia Darasani ifikapo January 15,205.
Kwa Upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Jiji la Dar es salaam Mwalimu Mussa Aly amewasihi Wazazi na Walezi waweze kuwa tayari kuwapeleka Watoto shuleni ili wakapate Elimu.
Ikumbukwe kuwa Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Amani ulianza kutekelezwa agost 16, 2022 na kutarajiwa kuzinduliwa January 15,2025 hivyo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1.
Hakuna maoni: