TANZANIA KUZINDUA TUZO ZA UTALII NA UHIFADHI DISEMBA 20 , 2024 MWAKA HUU.

Published from Blogger Prime Android App

Wizara ya maliasili na utalii Tanzania imesema kuwa itaendelea kuumga mkono juhudi za serikali chini ya Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Dkt.Hassan Abbas wakati akitangaza kufanyika kwa uzinduzi wa Tuzo ya utalii na uhifadhi itakayofanyika Disemba 20 ,2024 mwaka huu jijini Arusha ambapo Tanzania kwa mara ya kwanza itatoa Tuzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambao wanakumbukwa kwa kutoa mchango ulioiwezesha sekta hiyo ya kuwa na mafanikio makubwa


Katika hatua nyingine Dkt.Hassan abbas ameweza kuzungumzia Tuzo ambazo Nchi imezipata dunianí na afrika kiujumla amesema kuwa tuzo hizo imetokana na Taifa kuwa na vivutio Bora na ambavyo vimekuwa vikichangia pato la Taifa Katika nyanja mbalimbali za kiutalii na akatatolea mfano mbuga za wanyama kama Serengeti , Ruaha, Ngorongoro pamoja na kuwepo na makumbusho ya kale ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha Taifa kuwa kivutio katika suala zima la kuingiza watalii nchini

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.