TANZANIA NA SOMALIA ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTORI YA AFYA.

Published from Blogger Prime Android App
Na WAF-Mogadishu, Somalia

 Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mh. Jenista Mhagama, hii leo Disemba 19,2024 ameshiriki katika hafla ya kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya serikali za Somalia na Tanzania katika sekta ya afya.

Makubaliano haya yanajikita katika maeneo muhimu ambayo yataboresha ustawi wa raia wa nchi hizo mbili.

Sehemu kuu zinazozingatiwa ni pamoja na utaalamu bobevu, utaalamu wa juu, ubadilishanaji wa wataalamu wa afya kati ya nchi hizo mbili, na ujenzi wa uwezo kwa wahudumu wa afya.

Maeneo mengine muhimu ni pamoja na utafiti,uvumbuzi, upatikanaji wa bidhaa za afya, na huduma za afya za kidijitali.

Pia kutakuwa na umakini katika utalii wa matibabu, ubadilishanaji wa uzoefu, na usimamizi wa minyororo ya usambazaji wa bidhaa za afya, pamoja na jitihada za kupata rasilimali za kuboresha huduma za afya.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.