TCCIA NA CHEMBA YA KIMATAIFA YA DUBAI WASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO YA KIBAIASHARA.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App
Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mheshimiwa Seleman Jafo, ameweka wazi dhamira ya Tanzania kuvutia wawekezaji zaidi katika sekta muhimu kama madini, nishati, ujenzi, na utalii. Katika kongamano la biashara lililofanyika jijini Dar es Salaam, Jafo aliwahimiza wawekezaji kutoka Dubai na kwingineko kutumia fursa zilizopo nchini, hasa kuelekea maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027. Amesisitiza uwekezaji katika hoteli na miundombinu ya starehe ili kuimarisha sekta ya utalii.

Ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Biashara lililoandaliwa na Dubai International Chamber na Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania lilifanyika jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuchochea biashara na uwekezaji wa pande mbili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Bw. Vincent Bruno Minja, amesisitiza umuhimu wa nafasi ya Dubai kama lango la kimkakati kwa bidhaa za Kitanzania kufikia masoko ya dunia. 

Aidha, amebainisha sekta zenye fursa kubwa za ushirikiano, zikiwemo kilimo, utalii, nishati, na teknolojia. Minja aliweka bayana kuwa ushirikiano wa karibu kati ya makampuni ya Tanzania na Dubai utaimarisha maendeleo ya kiuchumi ya pande zote.


Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers, Mheshimiwa Mohammad Ali Rashed Lootah, ameeleza kuwa kongamano hilo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Dubai na Afrika. 

Lootah amesisitiza kuwa, kupitia ushirikiano huo, pande zote mbili zitafaidika kutokana na fursa mpya za biashara na uwekezaji, huku akitaja sekta kama kilimo, teknolojia, na miundombinu kuwa na nafasi kubwa ya kuchochea maendeleo ya pande hizo.

Thamani ya Biashara Kati ya Tanzania na Dubai

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, thamani ya biashara isiyohusisha mafuta kati ya Tanzania na Dubai ilikua kwa asilimia 9 mwaka 2023, kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.7. Pia, jumla ya makampuni 274 kutoka Tanzania yamesajiliwa kama wanachama wa Dubai Chamber of Commerce kufikia Septemba 2024, hatua inayoonyesha uhusiano wa karibu wa kibiashara kati ya pande hizo mbili.

Kongamano hilo lilimalizika kwa kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Dubai Chambers na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), hatua inayolenga kuongeza fursa za biashara, kubadilishana maarifa, na kuimarisha mazingira ya uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai.

Makubaliano hayo yanalenga kukuza ushirikiano kati ya makampuni ya Dubai na Tanzania kwa kupitia shughuli mbalimbali kama mikutano ya kibiashara, misheni za kibiashara, na matukio ya kibiashara. Pande zote mbili pia zitaimarisha kubadilishana maarifa na taarifa, kuchunguza fursa za uwekezaji, na kuweka mazingira bora ya ushirikiano wa kibiashara.
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.