


Na Mariam Muhando.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Wafanyabiashara wadowadogo kuacha kufanya Biashara Barabarani ili Jiji la Dar es salaam liweze kuwa safi na salama.
Mpogolo ametoa agizo hilo Disemba 9,2024 katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeadhimisha siku hii Kwa kufanya usafi katika Soko la Ilala liliopo Jijini hapa na kupanda miti kwenye Ufukwe wa Dengu.
"Tunapokwenda kuweka Jiji safi Viongozi tuache Siasa twendeni tukafanye kazi hili Jiji linatembelewa na wageni mbalimbalimbali tukahakikishe tunakwenda kutekeleza agizo la Viongozi wetu hivyo Watendaji wenzangu twendendeni tukasimamie sheria",Alisema Mpogolo.
Wakati huo huo amemtaka Mkurugenzi wa Jiji Elihuruma Mabelya ashirikiane na Viongozi wa Masoko katika kuanzisha mashindano ili kuimarisha Masoko mbalimbali yaliopo Jijini hapa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema watahakikisha mazingira yanatunzwa ili jiji la Dar es salaam liweze kuwa safi na salama kwa Binadamu hasa kwenye ulinzi wa afya na usalama wa mazingira.
"Tumejipanga kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira linakuwa kipaumbele katika Masoko yetu hivyo ajenda hii utaifanye iwe endelevu katika vikao vyetu",Alisema Mabelya.
Hakuna maoni: