Na Beatus Maganja,
Tabora.
Jumla ya watalii 770 kutoka viunga vya Mkoa wa Tabora na mikoa ya karibu wametembelea Bustani ya wanyamapori hai almaarufu TABORA ZOO Desemba 25, 2024 kujionea maajabu yaliyopo ndani ya bustani hiyo ikiwemo Nyumbu rafiki wa binadamu mwenye sifa za kipekee za kuambatana na watalii akiwaongoza katika vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya bustani hiyo iliyo chini ya usimamizi wa TAWA Mkoani Tabora.
TABORA ZOO ni bustani ya wanyamapori hai iliyosheni aina mbalimbali za wanyamapori kama vile tembo, fisi, pofu, Simba, Chui, Duma, Swala, Pundamilia, Ngiri na wengine wengi wakiwemo ndege nyuni wenye sauti za aina yake. Lakini kumekuwepo na mnyama nyumbu ambaye amejizolea umaarufu mkubwa hivi karibuni kiasi cha kupewa Jina "TOUR GUIDE" ambaye licha ya kuongoza watalii amekuwa akipenda sana kucheza na binadamu
TAWA inaendelea kuwakaribisha watanzania wote kutembelea Bustani hiyo ya aina yake kujionea urithi wa nchi yao
Hakuna maoni: